

Lugha Nyingine
Semina ya kibiashara kuhusu maonesho ya biashara ya Canton yavutia wazalishaji, viongozi wa biashara wa Ethiopia
Semina ya utangazaji bidhaa kwenye Maonesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Nje Bidhaa ya China, yanayojulikana pia kwa jina la Maonyesho ya Canton, imefanyika jana Alhamisi mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Semina hiyo iliwaleta pamoja maofisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, wawakilishi kutoka jumuiya ya wafanyabiashara wa Ethiopia na China, wajumbe wa China na wanadiplomasia wa China nchini Ethiopia.
Washiriki kwenye semina hiyo wamesema Maonyesho hayo ya Canton yana jukumu muhimu katika kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi zao na kwingineko.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na Mashirika ya Kisekta ya Ethiopia (ECCSA) Kenenisa Lemi, amesema Maonyesho ya Canton ni msingi wa muda mrefu wa maendeleo ya biashara duniani,akisema kuwa jumuiya yake iko tayari kuwezesha wafanyabiashara wa Ethiopia kushiriki kwenye maonyesho hayo yajayo, yaliyopangwa kufanyika kuanzia Aprili 15 hadi Mei 5 mjini Guangzhou, China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma