China na Botswana zasaini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi

(CRI Online) Februari 28, 2025

China na Botswana zimesaini makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi kati ya serikali zao jana Alhamisi mjini Gaborone.

Akiongea katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo, Balozi wa China nchini Botswana Bw. Fan Yong amesema China na Botswana zina urafiki mkubwa wa tangu zamani, na ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili umezaa matunda.

Amesema, kutokana na utekelezaji wa makubaliano na matokeo mengine ya mkutano wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali utaimarishwa zaidi.

Makamu wa Rais wa Botswana ambaye pia ni waziri wa fedha wa nchi hiyo, Bw. Ndaba Gaolathe amepongeza mafanikio makubwa iliyopata China na kushukuru uungaji mkono endelevu wa China kwa Botswana, akisema anatumai kuwa ushirikiano kati ya nchi yake na China utachangia ukuaji wa uchumi wa Botswana na maslahi ya watu wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha