

Lugha Nyingine
Mkutano wa Kamati ya Wajumbe wa Kudumu ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China wafungwa
Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akiongoza na kutoa hotuba kwenye mkutano wa 10 wa Kamati ya wajumbe wa kudumu ya Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC uliofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 2. (Xinhua/Xie Huanchi)
BEIJING - Kamati ya 14 ya kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambayo ni chombo cha kitaifa cha China cha mashauriao ya kisiasa, imemaliza mkutano wa kumi wa kamati yake ya wajumbe wa kudumu mjini Beijing jana Jumapili. Wang Huning, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya CPPCC, aliongoza na kutoa hotuba kwenye mkutano huo.
“Kamati ya Kitaifa ya CPPCC ilijikita katika majukumu makuu ya Chama na nchi kutekeleza wajibu mwaka jana na kupata mafanikio mapya katika kazi zake mbalimbali,” Wang amesema.
Ametoa wito kwa chombo hicho cha mashauriano ya kisiasa kutoa mchango mwaka 2025 ili kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na kufikia kwa sifa bora malengo na majukumu yaliyowekwa katika Mpango wa 14 wa Maendeleo ya Uchumi na Jamii ya Miaka Mitano wa China.
Wang pia amehimiza juhudi za kuhakikisha mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya kitaifa ya CPPCC unafanyika kwa mafanikio.
Mkutano huo wa wajumbe wa kudumu uliomalizika jana umepitisha nyaraka kadhaa zikiwemo mswada wa ajenda na ratiba ya mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya kitaifa ya CPPCC, ripoti ya kazi ya Kamati ya wajumbe wa kudumu ya Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC, na ripoti kuhusu kazi ya kushughulikia mapendekezo yaliyotolewa na washauri wa kisiasa tangu mkutano wa pili wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC.
Nyaraka hizo zitawasilishwa kwenye mkutano wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC kwa mapitio.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma