Shule inayosaidiwa na China yafanya vizuri katika mitihani ya taifa ya Botswana kwa mwaka wa pili mfululizo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2025

Konsuli wa Ubalozi wa China nchini Botswana Cui Yin (wa nne, kulia) akipiga picha na wanafunzi wenyeji wakati akihudhuria sherehe katika Shule ya Msingi Mmopane inayosaidiwa na China katika Wilaya ya Kweneng, Botswana, Februari 28, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Konsuli wa Ubalozi wa China nchini Botswana Cui Yin (wa nne, kulia) akipiga picha na wanafunzi wenyeji wakati akihudhuria sherehe katika Shule ya Msingi Mmopane inayosaidiwa na China katika Wilaya ya Kweneng, Botswana, Februari 28, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Shule ya Msingi Mmopane nchini Bostwana inayosaidiwa na China imefanya vizuri katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi, ikishika nafasi ya kwanza katika Wilaya ya Kweneng, kusini mwa nchini hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo kwa kupata ufaulu wa asilimia 94.3.

Kwenye sherehe iliyofanyika Ijumaa katika Kijiji cha Mmopane, umbali wa kilomita takriban 15 kaskazini-magharibi mwa Gaborone, mji mkuu wa Botswana, Konsuli wa Ubalozi wa China nchini Botswana Cui Yin ameipongeza shule hiyo kwa matokeo yake hayo bora katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Mwaka 2024.

"Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Botswana. Ubalozi wa China utaendelea kuimarisha ushirikiano wa kielimu na Botswana ili kuhimiza mafanikio zaidi," amesema, akielezea matumaini yake kwamba watoto wa Botswana watakuwa wawakilishi vijana wa urafiki kati ya China na Botswana na kuchangia katika kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.

Helen P. Manyeneng, naibu spika wa Bunge la Botswana, ameishukuru serikali ya China kwa kujenga Shule hiyo ya Msingi Mmopane na kutoa usaidizi muhimu kwa maendeleo yake. Amesema shule hiyo imeboresha kwa kiasi kikubwa hali ya elimu ya Mmopane na kutoa uungaji mkono mkubwa kwa ukuaji wa watoto wenyeji.

Gagoitsiwe Marata, mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Mmopane, ametoa shukrani kwa Ubalozi wa China kwa uungaji mkono wake wa kila mara, vilevile kwa serikali ya Botswana. Pia ametambua ari na uhimilivu wa walimu, wazazi na wanafunzi katika kuchangia ufaulu wa shule hiyo.

Mbali na shule hiyo ya Mmopane, China pia imesaidia Shule ya Msingi Ramaeba iliyoko Kazungula, Shule ya Msingi Kubung iliyoko Maun, na Shule ya Msingi Dinokwane iliyoko Serowe nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha