Kenya yapambana na moto wa msituni katika mbuga zake huku kukiwa na ukame mkali

(CRI Online) Machi 03, 2025

Vikosi vya dharura vya Kenya, vinavyojumuisha vikosi vya ulinzi na watu wa kujitolea, vimezidisha juhudi za kuzuia moto uliosambaa katika baadhi ya mbuga zake kubwa za wanyamapori na maeneo ya hifadhi nchini humo.

Taarifa ya hivi punde kutoka Shirika la Wanyamapori la Kenya (KWS), iliyotolewa Ijumaa jioni mjini Nairobi, imesema moto huo mkali uliozuka katika mbuga nyingi za wanyamapori zikiwemo Mbuga ya Taifa ya Nairobi na Hifadhi ya Taifa ya Aberdare pamoja na maeneo mengine ya bioanuwai unahusishwa na ukame mkali.

KWS imesema kwa sasa juhudi za kuzima moto huo zinaendelea, na kuongeza kuwa magari yenye matangi ya maji yako kwenye eneo la tukio ili kusaidia kuzima moto huo.

Aidha KWS imepeleka helikopta na timu za ardhini kukabiliana na janga hilo, ambalo limehusishwa na ukame mkali nchini humo.

Mfumo wa ikolojia wa Mlima Kenya ulio katikati mwa Kenya, ambao ni makazi ya viumbe mashuhuri kama vile tembo, faru na nyati, pia umeteketezwa na moto huo uliochochewa na upepo mkali na mimea iliyokauka.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha