Rais wa Tanzania apongeza kuongezeka kwa kasi ya usafirishaji wa mizigo katika Bandari ya Tanga iliyoboreshwa na China

(CRI Online) Machi 03, 2025

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema bandari ya Tanga iliyoboreshwa na kampuni ongozi ya Uhandisi wa Bandari ya China, sasa inahudumia tani zaidi ya milioni 1.2 za mizigo kwa mwaka, ikiwa ni ongezeko la tani 400,000 kwa mwaka kutoka uwezo wa awali.

Akihutubia taifa siku ya Ijumaa mwishoni mwa ziara yake mkoani Tanga, Rais Samia amebainisha kuwa uboreshaji wa bandari hiyo umeongeza ufanisi wake kwa kiasi kikubwa, na kutoa ajira kwa vijana wenyeji, huku pia mipango ikitekelezwa kuigeuza bandari hiyo kuwa kitovu maalumu cha kuhudumia mbolea na mazao ya kilimo.

Oktoba 2024, Kaimu Meneja wa Bandari hiyo ya Tanga, Donald Gaile, alisema uboreshaji huo umehusisha uchimbaji na ujenzi wa magati yenye urefu wa mita 450, ambayo sasa yanaruhusu meli kutia nanga moja kwa moja kwenye gati na kushusha mizigo.

Gaile aliongeza kuwa bandari hiyo sasa inaweza kubeba meli zinazobeba tani zaidi ya 100,000 za mizigo kutoka duniani kote.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha