Bidhaa Bora za Afrika zaharakisha kuingia kwake kwenye soko la China katika Eneo la Majaribio ya Ushirikano wa Kina wa Kibiashara wa China-Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 03, 2025

Wakala wa chai ya zambarau ya Kenya (wa kwanza kulia) akitambulisha chai hiyo kwa washiriki maonesho kwenye Maonesho ya tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika. (Yang Xun, Dong Yuanjun/People’s Daily)

Wakala wa chai ya zambarau ya Kenya (wa kwanza kulia) akitambulisha chai hiyo kwa washiriki wa maonesho kwenye Maonesho ya tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika. (Yang Xun, Dong Yuanjun/People’s Daily)

Asubuhi, wavuvi kwenye pwani ya Kenya hutandaza nyavu zao za uvuvi baharini. Dagaa wanaowavua watachakatwa hadi kuwa samaki wakavu na kuuzwa nje nchini China, kufanywa kuwa vyakula vitamu na kusambazwa katika nchi zaidi ya 30.

Kampuni inayohusika na biashara hiyo ya kimataifa ni Kundi la Kampuni za Vyakula la Hunan Jinzai, ambayo kwa sasa imekuwa moja wa waagizaji wakubwa wa dagaa wakavu wa Kenya. "Mauzo yetu ya mwaka ya bidhaa husika yamepita yuan bilioni 1” (Dola za Marekani milioni 137 hivi) amesema Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Zhou Jinsong.

Tangu kutangazwa kwa "Mpango wa Jumla wa Ujenzi wa Eneo la Majaribio ya Ushirikiano wa Kina wa Kiuchumi na Biashara kati ya China na Afrika" Januari 2024, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara wa mkoa wa Hunan wa China na nchi za Afrika umeendelea kuongezeka. Kwa mujibu wa takwimu za Forodha ya Mji wa Changsha, mji mkuu wa Hunan, thamani ya biashara ya mkoa huo wa Hunan na nchi za Afrika mwaka 2024, ilikuwa yuan bilioni 54.85 (Dola za Marekani bilioni 7.53 hivi).

Kituo cha biashara ya kahawa na karanga za Afrika nchini China

Ukihimizwa na kuanzishwa kwa Eneo la Majaribio ya Ushirikiano wa Kina wa Kiuchumi na Biashara kati ya China na Afrika, Mkoa wa Hunan umejenga vituo vitatu vikuu vya kibiashara vya bidhaa za kahawa, karanga, na kilimo za Afrika. Bidhaa maalum za ubora wa juu za Afrika kama vile asali, karanga, soya, na matunda zimepata mauzo mazuri ya nje kwenye soko la China.

Shukrani kwa ufunguaji wa China wa "njia ya kijani" kwa bidhaa za kilimo za Afrika na kutekeleza hatua za uidhinishaji wa karantini wa forodha kama vile ukaguzi wa haraka, ukaguzi wa kipaumbele, na njia za ukaguzi wa kuidhinisha kwa haraka, kampuni ya Jing Jianhua "Xiao Ka Zhu" inayouza kahawa ya Afrika imefungua maduka zaidi ya 50 kote China.

Kwa mujibu wa takwimu za Forodha ya China, mwaka 2024, thamani ya biashara ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa wa China kwa Afrika ilifikia yuan trilioni 2.1, ongezeko la asilimia 6.1 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Teknolojia yaunga mkono maendeleo ya kilimo cha Afrika

Kampuni ya teknolojia ya hali ya juu ya kilimo ya Yuan Longping (Longping High-Tech) hutumia Maonesho ya Kiuchumi na Biashara ya China na Afrika (CAETE) kama jukwaa. Kwa sasa imefanya zaidi ya vipindi 200 vya mafunzo ya teknolojia ya kilimo katika nchi 53 za Afrika zikiwemo Kenya na Tanzania, na kuwapa mafunzo maafisa na wataalamu wa kilimo zaidi ya 7,000.

Naibu Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Longping High-Tech, Weng Yong anaamini kuwa, ni kupitia tu kuchagua na kuzalisha aina bora za mbegu, na kisha kutoa ujuzi wa mbinu bora za kilimo ndipo mfumo wa kilimo wenye nguvu na stahimilivu zaidi unaweza kujengwa kwa nchi za Afrika.

Jukwaa la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika

Maonyesho ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yameshafanyika kwa mafanikio mara tatu mkoani Hunan. Kwa kutumia ukumbi wa kudumu wa maonesho hayo na majukwaa mengine, eneo la Yuhua katika Eneo la Biashara Huria la Hunan linaonesha na kuuza bidhaa kutoka nchi 53 za Afrika. Mwaka 2024, uagizaji nje bidhaa za kilimo na chakula kama vile mihogo, mananasi, na parachichi kutoka Afrika ulianza nchini China.

Mwezi Juni mwaka huu, Maonyesho ya Nne ya Kiuchumi na Biashara ya China na Afrika yatafanyika mjini Changsha, Hunan. Waziri wa Biashara, Uwekezaji, na Viwanda wa Kenya, Rebecca Miano, anaamini kuwa ushirikiano wa kiuchumi na biashara kati ya China na Afrika huweka msingi wa kunufaishana na manufaa ya pande zote mbili, na kusaidia China na nchi za Afrika kusonga mbele kuelekea mustakabali wa siku za baadaye ulio endelevu na uwezo mkubwa zaidi wa ushindani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha