

Lugha Nyingine
Mwelekeo wa maendeleo mazuri ya muda mrefu ya uchumi wa China haujabadilika
Liu Jieyi, msemaji wa Mkutano wa Tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), akihudhuria mkutano na waandishi wa habari kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 3, 2025. (Xinhua/Li He)
BEIJING - Msemaji wa Mkutano wa Tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, ambalo ni chombo kikuu cha mashauri ya kisiasa cha China, Liu Jieyi, amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatatu kwamba hali ya msingi na mwelekeo wa kimsingi wa maendeleo mazuri ya muda mrefu ya uchumi wa China bado haujabadilika.
Liu amesema uchumi wa China una msingi imara, nguvu bora mbalimbali, uhimilivu mkubwa na uwezo mkubwa, na ina nguvu bora za kipekee za mifumo, soko la ndani lenye ukubwa wa kupita kiasi na mfumo kamili wa viwanda.
Msemaji huyo amekiri kuwa mazingira ya ndani na nje ya China, na maendeleo ya uchumi wa China bado yanakabiliwa na changamoto na mambo magumu mengi, mahitaji ya ndani bado hayajatosha na hatari katika baadhi ya maeneo bado hazijaondolewa.
Ametoa wito wa kutoa nguvu zote kukabiliana na mambo hayo magumu na kudumisha imani, na amesisitiza kuwa maendeleo ya sifa bora ya uchumi hakika yatapanda ngazi mpya.
“Nchi ya China imeapa kuhimiza ufunguaji mlango katika maeneo mengi zaidi na kwa kina zaidi,” msemaji huyo ameeleza.
Amesema China itaendelea kupanua ufunguaji mlango wa kimfumo kwa hatua madhubuti, kuzidisha mageuzi ya muundo wa biashara ya nje, kuboresha mpangilio wa ufunguaji mlango wa kieneo kwa nje, na kukamilisha mfumo wa ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.
“Katika mwaka uliopita, China imezidisha ufungamanishaji wa uvumbuzi wa kiteknolojia na uvumbuzi wa kazi za viwanda, kuharakisha uhimizaji wa mambo ya kisasa kwenye mfumo wa viwanda, na kupata mafanikio dhahiri katika kuendeleza nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora” Liu amesema.
Amesema kuwa nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora zinatumika kama injini imara kwa maendeleo ya sifa bora ya China, Liu ametoa wito wa kuendelea kufanya juhudi na kuongeza zaidi ari ya watu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma