

Lugha Nyingine
Mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China kuanza leo Machi 4 hadi 10
BEIJING - Mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), ambalo ni chombo kikuu cha kutoa mashauri ya kisiasa cha China utafanya mkutano wake wa mwaka kuanzia leo Jumanne, Machi 4 hadi 10 mjini Beijing, msemaji wa mkutano huo amesema jana Jumatatu.
“Mkutano huo wa tatu wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya CPPCC umepangwa kuanza leo Jumanne saa 9 mchana (kwa saa za Beijing) na kufungwa asubuhi ya Machi 10,” msemaji Liu Jieyi amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Msemaji huyo amesema, wakati wa mkutano huo wa mwaka, washauri wa kisiasa wa kitaifa wa China watasikiliza, kujadili na kupitisha ripoti ya kazi ya Kamati ya Wajumbe wa Kudumu ya CPPCC na ripoti juu ya kazi ya kushughulikiwa kwa mapendekezo.
Ameongeza kuwa, wajumbe wa baraza hilo pia watahudhuria kwenye Mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China, ambalo ni chombo kikuu cha utungaji wa sheria, utakaofunguliwa kesho Jumatano, Machi 5, ambapo watasikiliza ripoti ya kazi ya serikali na ripoti nyingine husika. Baadaye watathibitisha ripoti na maazimio mbalimbali ya mkutano wa mwaka wa Baraza la Mashauriano ya kisiasa.
“Mkutano huo wa Mwaka 2025 wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa ukiwa ni pamoja na mkutano wa wajumbe wote, na majadiliano na mashauriano ya kikundi kikundi. Mabalozi wa nchi mbalimbali nchini China wataalikwa kama wasikilizaji kwenye ufunguzi na ufungaji wa mkutano,” amesema Liu.
“Katika mwaka uliopita, washauri wa kisiasa wa kitaifa wa China wamefanya juhudi zaidi za kufuatilia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, wakitoa mapendekezo na kuhimiza kufikia maelewano mapana,” amesema.
Ameeleza kuwa, wajumbe hao pia walitembelea vijiji, viwanda na maeneo ya wakazi, wakikusanya maoni na mapendekezo kutoka ngazi za mashinani na kuyafanya kuwa machaguo ya kisera, na kutoa habari mbalimbali kwa ajili ya Chama na serikali kutoa sera na maamuzi.
“Ili kuunga mkono ujenzi wa mambo ya kisasa, mageuzi na maendeleo ya sifa bora, na kuhakikisha hali ya maafikiano ya jamii, Baraza la Mashauriano ya Kisiasa lilianzisha miradi 42 ya utafiti kuhusu masuala makubwa, kufanya mashauriano na maamuzi 85, na kushughulikia mapendekezo zaidi ya 5,000 katika mwaka mmoja uliopita,” msemaji huyo ameeleza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma