

Lugha Nyingine
IMF yaanza kuhakiki masuala ya utawala nchini Kenya ili kushughulikia ufisadi na kuimarisha ufanisi wa kiuchumi
Mkuu wa Mawaziri wa Kenya ambaye pia ni Waziri wa Masuala ya Kigeni na Diaspora Musalia Mudavadi amesema Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Jumatatu lilianza kuhakiki rasmi masuala ya ufisadi na utawala nchini Kenya.
Katika taarifa iliyotolewa mjini Nairobi baada ya mkutano wake na Naibu Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Masuala ya Fedha ya IMF Rebecca A. Sparkman, Mudavadi amesema matokeo ya tathmini ya kiufundi yatawezesha serikali kutekeleza mageuzi ya kipaumbele cha utawala ili kupambana na ufisadi na kuunga mkono ukuaji wa uchumi.
Aidha amekaribisha mwitikio wa IMF juu ya ombi la serikali ya Kenya la kutaka kufanyiwa Tathmini ya Utawala, inayoanza na kazi ya uchunguzi na kufuatiwa na tathmini kamili baadaye mwaka huu.
Hatua ya kualika timu hiyo ya IMF imekuja baada ya Rais wa Kenya William Ruto, ambaye alishinikizwa na waandamanaji vijana wanaodai uwajibikaji, kuahidi kupendekeza mabadiliko ya sheria husika Julai 2024 ili kuziba mianya inayodhoofisha vita dhidi ya ufisadi.
Ruto alisema marekebisho hayo ya kisheria yatajumuisha kuchukulia hatua kali mafisadi na wale wanaoonesha utajiri na upotevu kwenye matumizi ya serikali huku kukiwa na gharama za juu za maisha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma