Tanzania kujenga vyuo 145 vya ufundi stadi kwa ajili ya maendeleo ya vijana

(CRI Online) Machi 04, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini Tanzania (VETA), CPA Anthony Kasore Jumatatu alisema, serikali ya Tanzania itajenga vyuo 145 vya VETA kabla ya mwisho wa mwaka 2025, ili kuwapatia vijana ujuzi na uwezo hitajika katika masoko ya ajira ya ndani na ya kimataifa.

Kasore amesema vyuo 80 vya VETA vimejengwa nchini humo na kwamba vinalenga kuandaa vijana wenye ujuzi wa kitaalamu, ambao wataendeleza uvumbuzi, ujasiriamali, na maendeleo endelevu ya kiuchumi.

CPA Kasore ameongeza kuwa kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2024, vijana takriban 295,175 wamejiandikisha kushiriki kwenye vyuo vya VETA, na kupata ujuzi na utaalamu wa kiufundi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha