Moto katika mbuga ya wanyama ya Nairobi nchini Kenya waelezwa kusababishwa na sigara

(CRI Online) Machi 04, 2025

Waziri wa Utalii na Wanyamapori nchini Kenya, Bi Rebecca Miano, amethibitisha kuwa moto ulioteketeza ekari 210 kati ya 28,000 katika mbuga ya Kitaifa ya Nairobi ulisababishwa na kipande cha sigara kilichotupwa karibu na hifadhi hiyo.

Akizungumza katika eneo la tukio, Waziri Miano amesema moto huo, ambao ulizuka majira ya saa kumi jioni kwa saa za huko katika eneo la Athi Basin karibu na Kitengela, ulizimwa kwa mafanikio kupitia juhudi za taasisi mbalimbali, ikiwemo Shirika la Huduma za Wanyamapori Kenya (KWS), Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), timu za serikali za kaunti, mashirika ya usalama, na wakazi wenyeji.

Waziri Miano amesifu mwitikio wa haraka ya vikosi vya kukabiliana na moto, akisisitiza kuwa hakuna mnyama yeyote aliyeripotiwa kuathiriwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha