

Lugha Nyingine
Tume Tendaji na ajenda za mkutano vyaandaliwa tayari kwa mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China
Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China Katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
BEIJING – Wajumbe wa Bunge la 14 la Umma la China wamekusanyika mjini Beijing siku ya Jumanne kwenye kikao cha matayarisho cha mkutano wa tatu wa bunge hilo la 14 la China utakaoanza leo Jumatano, ili kuchagua Tume Tendaji wa mkutano na kupanga ajenda zake.
Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China aliongoza kikao hicho cha maandalizi.
“Kazi zote za maandalizi ya mkutano huo wa mwaka zimekamilika,” Zhao amesema.
Kikao hicho kimewachagua wajumbe 176 kwa kuunda Tume Tendaji wa Mkutano, huku Li Hongzhong akiwa katibu mkuu wa mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China.
Kikao hicho cha maandalizi pia kimepitisha ajenda za mkutano huo wa mwaka wa bunge zikiwemo pamoja na kuthibitisha ripoti ya kazi ya serikali, ripoti ya utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa mwaka 2024, mswada wa mipango ya mwaka 2025, na mswada wa mpango wa maendeleo ya uchumi na jamii wa mwaka 2025.
Tume Tendaji iliyochaguliwa ilifanya kikao kingine baada ya kikao hicho cha maandalizi kumalizika. Wajumbe wa tume waliohudhuria kikao hicho kilichofuata wameamua ratiba ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14, pamoja na mambo mengine. Mkutano huo wa bunge utaanza kuanzia leo Machi 5 hadi 11 mwaka huu.
Kabla ya kikao hicho cha maandalizi, Baraza la Wenyeviti wa Kamati ya Wajumbe wa Kudumu ya Bunge la 14 liliitisha kikao cha kufanya maandalizi.
Mwenyekiti wa Bunge la Umma Zhao Leji ameongoza mkutano wa Tume ya Utendaji wa mkutano na kikao cha Baraza la Wenyeviti.
Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akiongoza kikao cha kwanza cha Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Zhao Leji, mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, akiongoza Mkutano wa 41 wa Baraza la Wenyeviti wa Bunge la 14 la Umma la China katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 4, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma