

Lugha Nyingine
China yatoa waraka juu ya vitu vinavyohusika na fentanyl na kusisitiza udhibiti mkali
BEIJING -Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka wenye kichwa "Kudhibiti Vitu Vinavyohusika na Fentanyl - Mchango wa China," ukionyesha udhibiti mkali wa China juu ya kemikali hizo.
China imekuwa ikiweka umuhimu mkubwa katika kudumisha udhibiti wa vitu vinavyohusika na fentanyl katika miaka ya hivi karibuni, waraka huo uliotolewa jana Jumanne unasema.
Waraka huo unaeleza kuwa, China imetekeleza usimamizi mkali juu ya dawa zinazohusika na fentanyl, ikizuia vikali matumizi mabaya ya vitu vinavyohusika na fentanyl, na imekuwa ikipambana vikali na shughuli za magendo, utengenezaji, na usafirishaji haramu wa vitu vinavyohusika na fentanyl na kemikali husika za awali.
" Kazi hizi zimeleta matokeo makubwa," waraka unasema.
Waraka huo pia unasisitiza dhamira ya China ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kuhusu udhibiti wa dawa za kulevya kwa njia ya mazungumzo, uchunguzi wa pamoja, na kunufaika pamoja na ujuzi husika, huku ikihimiza uhusiano wa washirika kwenye msingi wa kuwa na usawa na kuaminiana.
"China imepata mafanikio makubwa katika ushirikiano wa kina na nchi husika, ikiwa ni pamoja na Marekani, katika kushughulikia matatizo ya vitu vinavyohusika na fentanyl na vitu vitangulizi vyake," waraka huo unasema.
Kwa mujibu wa waraka huo, China imeziweka dawa zinazohusika na fentanyl kwenye Orodha ya Dawa za Kulevya Zinazodhibitiwa na inafanya udhibiti mkali juu ya utengenezaji na uuzaji wake, matumizi na uuzaji wake nje.
“Kuhusu udhibiti, China imefanya juhudi kubwa za kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji wa kidijitali wa dawa zinazohusika na fentanyl,” waraka huo umesema.
China imetumia njia za jumla za teknolojia na mbinu mpya, kama vile alama za utambuzi wa masafa ya redio, mtandao wa Intaneti wa vitu na teknolojia ya AI ikitimiza ufuatiliaji makini na usimamizi wa jumla wa mchakato mzima juu ya utengenezaji, uuzaji, usafirishaji, matumizi, uagizaji na uuzaji nje wa dawa zinazohusika na fentanyl, ili kuzuia zaidi zisipotee.
“China inafanya juhudi za kukabiliana na changamoto mpya zinazotokana na vitu vinavyohusika na fentanyl,” unasema waraka huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma