

Lugha Nyingine
Mkutano wa mwaka wa Bunge la Umma la China wafunguliwa
(CRI Online) Machi 05, 2025
(Ding Haitao/Xinhua)
Mkutano wa Tatu wa Bunge la 14 la Umma la China (NPC) umefunguliwa leo Jumatano kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, ambapo wajumbe takriban 3000 kutoka maeneo, makabila na sekta mbalimbali kote nchini humo wanahudhuria.
Wakati wa mkutano huo wa wiki moja, wajumbe watasikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali, kuhitimisha matokeo ya kazi yaliyopatikana katika mwaka uliopita na kuweka mipango kuhusu maendeleo ya nchi hiyo katika mwaka mpya.
Vilevile mkutano huo utakagua ripoti kuhusu mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ripoti kuhusu bajeti ya serikali kuu na ya mikoa, na ripoti kuhusu kazi za Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma