Rais wa Ghana aanzisha mazungumzo ya kitaifa juu ya ukuaji wa kiuchumi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 05, 2025

Rais wa Ghana John Dramani Mahama (wa sita, kulia) na washiriki wengine wa mazungumzo ya kitaifa ya kiuchumi wakiwa katika picha ya pamoja mjini Accra, Ghana, tarehe 3 Machi 2025. (Xinhua/Seth)

Rais wa Ghana John Dramani Mahama (wa sita, kulia) na washiriki wengine wa mazungumzo ya kitaifa ya kiuchumi wakiwa katika picha ya pamoja mjini Accra, Ghana, tarehe 3 Machi 2025. (Xinhua/Seth)

ACCRA - Rais wa Ghana John Dramani Mahama amezindua mazungumzo ya kitaifa ya kiuchumi siku ya Jumatatu wiki hii ili kuangalia njia ya ukuaji wa kiuchumi wa nchi hiyo, ambapo akihutubia washiriki katika mji mkuu wa taifa hilo, Accra, Mahama amesisitiza umuhimu wa mkutano huo ambao utatafuta suluhu kwa changamoto za kiuchumi za Ghana zinazojirudia mara kwa mara na kuandaa mikakati ya kuirejesha nchi hiyo katika njia ya ukuaji endelevu.

“Tumekusanyika hapa ili kurudisha nguvu ya uchumi wa nchi yetu ili kutufanya kuwa kinara wa upigaji hatua katika Bara la Afrika, si tu kuwa kinara wa demokrasia bali kinara wa ustawi wa kiuchumi,” amesema.

Rais huyo amesisitiza mchango muhimu wa mageuzi ya utawala ili kuboresha uwazi na uwajibikaji, akihimiza uwajibikaji wa pamoja katika kujenga upya uchumi. "Ninaapa kufanya kila niwezalo kuliongoza taifa hili kuelekea mustakabali mzuri na wenye ustawi zaidi," amesema.

Mahama pia ametoa wito wa mapendekezo ya mageuzi ya kimuundo ambayo yatashughulikia mahitaji ya sekta binafsi ili kuifanya kuwa injini halisi ya ukuaji wa kutengeneza ajira kwa vijana wanaoongezeka.

"Njia kuelekea kuimarisha uchumi itakuwa na changamoto, lakini hatupaswi kulegea katika nia yetu ya kuijenga upya Ghana tunayoitaka sote. Nina dhamira ya kuhakikisha kwamba mafunzo tuliyojifunza kutokana na mazungumza haya yatabadilisha maamuzi tunayofanya katika miaka ijayo," ameongeza.

Chini ya kaulimbiu ya "Kuiweka upya Ghana: Kujenga Uchumi Tunaotaka Pamoja," mazungumzo hayo ya siku mbili yamewakutanisha pamoja maafisa wa serikali, viongozi wa biashara, washirika wa maendeleo, vyama vya wafanyakazi, na watendaji wengine.

Nchi hiyo muuzaji nje wa kakao, dhahabu na mafuta ghafi kutoka Afrika Magharibi imekuwa akitekeleza mageuzi ya kiuchumi tangu Mei 2023, yakiungwa mkono na mkopo wa dola za Kimarekani bilioni 3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa ili kukabiliana na changamoto nyingi za kiuchumi, zikiwemo za kushuka kwa thamani ya sarafu, mfumuko wa bei na kuongezeka kwa madeni ya sekta ya umma.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha