

Lugha Nyingine
Mkutano wa kutangaza Maonyesho ya Canton wafanyika Kenya
Mkutano wa kutangaza Maonyesho ya 137 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China, ambayo pia yanafahamika kwa jina la Maonyesho ya Canton, umefanyika Jumanne mjini Nairobi nchini Kenya, ukiwaleta pamoja watunga sera waandamizi, maofisa watendaji wa kampuni na wajasiriamali.
Mkutano huo umeandaliwa na Kituo cha Biashara ya Nje cha China, Ubalozi wa China nchini Kenya, na Kampuni ya Mawasiliano ya Habari na Utamaduni ya China nchini Kenya (CICCK).
Mkurugenzi wa opresheni wa Kituo cha Biashara ya Nje cha China Bw. Xu Jiansheng amesema Maonyesho ya 137 ya Canton yatakayofanyika kuanzia tarehe 15 Aprili hadi tarehe 5 Mei yataimarisha zaidi hadhi ya China kama kitovu cha biashara duniani pia yatahimiza mawasiliano ya kirafiki kati ya China na sehemu nyingine duniani.
Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya anayeshughulikia mambo ya kuhimiza uwekezaji na maendeleo ya biashara Pius Rotich amesema Maonyesho ya Canton yanatoa fursa ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kuvutia mitaji na teknolojia kutoka China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma