

Lugha Nyingine
China yatangaza lengo himilivu la ukuaji wa uchumi kwa uungaji mkono imara wa sera
BEIJING - China imeweka lengo la ukuaji uchumi la karibu asilimia 5 kwa mwaka 2025, ikionyesha mtazamo mzuri wa kiuchumi licha ya kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika duniani, kwani watunga sera wa nchi hiyo wamedhamiria kuhakikisha uchumi unaimarika kwa utulivu kupitia hatua madhubuti yenye ufanisi.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Li Qiang Jumatano alitangaza lengo hilo wakati akitangaza ripoti ya kazi ya serikali kwenye mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China unaondelea mjini Beijing kwa ajili ya kujadiliwa.
Ripoti hiyo imeeleza malengo mengine muhimu ya maendeleo kwa mwaka huu, yakiwemo kudhibiti kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilichotafitiwa kuwa karibu asilimia 5.5, kutoa nafasi mpya za ajira za mijini zaidi ya milioni 12, na kuwa na ongezeko la karibu asilimia 2 katika Kiwango cha bei za vitu vya watumiaji wa China (CPI).
Picha hii ikionyesha banda la Kampuni ya Kiteknolojia ya Contemporary Amperex kwenye Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Magari ya Guangzhou katika Jumba la Maonyesho ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China mjini Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Novemba 15, 2024. (Xinhua/Deng Hua)
China ilipata ukuaji wa uchumi wa asilimia 5 katika kipindi cha mwaka 2024 wakati ambapo kifurushi cha sera chenye mchango mkubwa, pamoja na hatua zingine za kuunga mkono ukuaji uchumi, zilisaidia kusukuma mbele mwelekeo wa ongezeko la uchumi.
Huku mwaka 2025 ukiwa ni mwaka wa mwisho wa Mpango wa 14 wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa China (2021-2025) na ni muhimu kwa kuandaa mpango mwingine wa miaka mitano ijayo, wachunguzi wa mambo wanaamini kwamba sera za serikali si tu zitachochea ukuaji endelevu mwaka huu bali pia zitaweka msingi wa kusukuma ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi hiyo katika muda mrefu.
Lengo lenye mantiki, lenye kufikika
Kwa nini serikali ya China imedumisha lengo la ukuaji wa uchumi kwa karibu asilimia 5?
Waziri Mkuu Li ameeleza kuwa lengo hilo, likiungwa mkono na uwezo wa ukuaji na hali nzuri, linakidhi hitaji la kuimarisha hali ya ajira, kuzuia hatari na kuboresha ustawi wa watu, huku pia likiendana vyema na malengo ya kati na ya muda mrefu ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, China itapitisha sera kuhusu matumizi ya fedha ya kuchochea hamasa zaidi na sera ya fedha iliyolegea kwa kiasi kinachofaa.
Picha iliyopigwa Januari 6, 2025 ikionyesha kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua cha Shichengzi katika Mji wa Hami, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China. (Picha na Feng Yang/Xinhua)
Picha hii iliyopigwa Novemba 13, 2024 ikionyesha vitu vinavyohusiana na uchumi wa anga ya chini kwenye Maonyesho ya Vyombo vya Usafiri wa Anga ya China mjini Zhuhai, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China. (Xinhua/Liang Xu)
Mtu akitumia programu ya DeepSeek kwenye simu ya mkononi Februari 17, 2025. (Xinhua/Huang Zongzhi)
Uhai na Uendelevu Zaidi
Kuhimiza maendeleo ya hali ya juu ni lengo kuu katika ajenda ya serikali ya China mwaka huu, huku vipaumbele vikianzia kuchochea mahitaji ya ndani katika manunuzi hadi kuunda nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora.
"Tutachukua hatua zinazowapa kipaumbele watu na kuweka mkazo wa sera ya uchumi katika kuboresha viwango vya maisha na kuongeza matumizi ya wanunuzi," Waziri Mkuu Li amesema.
Wateja wakifahamishwa kuhusu sera husika wakati wa shughuli ya kubadilisha bidhaa mpya kwa bidhaa za awali katika Mji wa Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Mei 17, 2024. (Xinhua/Li Ziheng)
Ripoti hiyo imesema mahitaji ya ndani yatakuwa injini kuu na nanga ya kutuliza ukuaji wa uchumi, huku ikieleza kuwa dhamana maalum za serikali za muda mrefu zenye thamani ya jumla ya Yuan bilioni 300 zitatolewa kwa ajili ya kuunga mkono mipango ya kubadilisha bidhaa mpya kwa bidhaa za awali.
Nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora zitakuzwa kulingana na hali ya eneo husika, ripoti hiyo imeeleza, ikiongeza kuwa, China inalenga kukuza tasnia zinazoibukia na za siku za baadaye, kama vile teknolojia ya quantum na uchumi wa anga ya chini, kuharakisha uboreshaji wa viwanda vya jadi, na kuunganisha teknolojia za kidijitali kama vile AI na nguvu za viwanda na soko.
Watu wakitazama filamu ya "Ne Zha 2" katika 4D kwenye ukumbi wa sinema katika Eneo la Dongcheng mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 16, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)
Watu mjini Lhasa, China wafanya maandalizi ya sikukuu ijayo ya Mwaka Mpya wa Watibet
Mandhari na wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, Kenya
Habari Picha: Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja mjini Haikou, China
Dunhuang katika Mkoa wa Gansu wa China yakaribisha maendeleo mapya
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma