Daktari wa China aacha historia ya kudumu nchini Zimbabwe kupitia dawa za jadi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2025

Hu Sha, daktari wa matibabu za kijadi za Kichina kutoka timu ya 21 ya madaktari wa China nchini Zimbabwe, akimtibu mgonjwa mwenyeji mjini Harare, Zimbabwe, Februari 27, 2025. (Xinhua/Tafara Mugwara)

Hu Sha, daktari wa matibabu za kijadi za Kichina kutoka timu ya 21 ya madaktari wa China nchini Zimbabwe, akimtibu mgonjwa mwenyeji mjini Harare, Zimbabwe, Februari 27, 2025. (Xinhua/Tafara Mugwara)

HARARE - Baada ya miaka miwili ya huduma ya kujitolea, Hu Sha, daktari wa matibabu ya kijadi ya Kichina (TCM) anajiandaa kurejea China. Hata hivyo, anapoaga, anaacha historia ya kudumu nchini Zimbabwe, ambako kazi yake hiyo imegusa maisha ya watu wengi.

Licha ya kukumbuka nyumbani mara kwa mara, kuona wagonjwa wake wakipata nafuu ya ugonjwa kumekuwa kukimtia moyo.

"Ninapoona wagonjwa wangu walioumwa wakitabasamu tena, ninaposikia mtoto mwenyeji mwenye mtindio wa ubongo akisema 'asante' kwa lugha ya Kichina, najua juhudi zangu zote zimekuwa na manufaa," Hu ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Huku akijulikana kwa mchango wake kama Dokta “Chipo”, neno ambalo lina maana ya "zawadi" katika lugha ya Kishona ya Zimbabwe, Hu ametumia miaka miwili iliyopita kutoa mchango mkubwa kwa maisha ya wagonjwa katika Kituo cha TCM na Tiba ya Acupuncture cha Zimbabwe-China, kilichoko katika Hospitali ya Parirenyatwa mjini Harare, Zimbabwe.

"Ninaamini Zimbabwe na watu wake ni zawadi kwangu," amesema. "Imani yao kwa TCM na madaktari wa Wachina ni zawadi bora zaidi ambayo nimepokea katika miaka miwili iliyopita."

Hu ambaye aliwasili Zimbabwe kwa mara ya kwanza Machi 2023 kama daktari wa timu ya maktari wa China, awali kwa huduma ya mwaka mmoja. Kwa kuhamasishwa na kuongezeka kwa mchango wa TCM, aliamua kuongeza muda wake wa kubaki nchini humo kwa mwaka mwingine ili kuendelea kutoa huduma muhimu.

Kama mkuu wa kituo cha TCM, amekuwa akisimamia shughuli za kila siku, uhudumiaji wagonjwa, mafunzo, na uenezaji utamaduni wa TCM. Kuongezeka kukubalika kwa TCM miongoni mwa Wazimbabwe kumezidi matarajio yake.

"Mchango wa kiajabu wa uponyaji wa dawa za kijadi za Kichina umeenea sana nchini Zimbabwe, na idadi ya wagonjwa inaendelea kuongezeka. Miadi katika kituo cha TCM sasa imepangwa hadi Aprili," amesema.

Mwaka jana, kwa uungaji mkono wa kiufundi na kifedha wa Hospitali ya Kwanza ya Chuo Kikuu cha Tiba za Kichina cha Hunan katika Mkoa wa Hunan, China, Hu alianzisha chumba cha kwanza cha dharura cha TCM barani Afrika na chumba cha maonyesho kwenye kituo hicho.

Kwa Rudo Gonyora, mama wa mtoto mwenye umri wa miaka minne mwenye ugonjwa wa mtindio wa ubongo, acupuncture imesaidia kuboresha hali ya mtoto wake.

"Tangu tuanze matibabu ya acupuncture, amekuwa mchangamfu zaidi, akibubujikwa na nguvu, na mijongeo yake imeboreka. Udhibiti wa kichwa chake unakuwa bora. Tunaweza kuona maendeleo ya kweli," amesema.

Wenzake wenyeji katika kituo hicho cha TCM pia wamenufaika na uwepo wa Hu.

"Kuanzia watoto hadi watu wazima, aliwatendea kila mgonjwa kwa upendo na huruma," Charlotte Muziri, msaidizi katika kituo hicho amesema. "Amekuwa baraka ya kweli kwa kliniki yetu."

Xiao Zhiqiang, daktari wa matibabu ya kijadi ya Kichina kutoka timu ya 22 ya madaktari wa China nchini Zimbabwe, akimtibu mgonjwa mwenyeji mjini Harare, Zimbabwe, Februari 27, 2025. (Xinhua/Tafara Mugwara)

Xiao Zhiqiang, daktari wa matibabu ya kijadi ya Kichina kutoka timu ya 22 ya madaktari wa China nchini Zimbabwe, akimtibu mgonjwa mwenyeji mjini Harare, Zimbabwe, Februari 27, 2025. (Xinhua/Tafara Mugwara)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha