Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa utalii wa G20

(CRI Online) Machi 06, 2025

Afrika Kusini iliandaa mkutano wa kwanza wa kikosi kazi cha utalii wa Kundi la G20 kwa njia ya video siku ya Jumatano, ukikutanisha maofisa waandamizi, vyombo vya kiserikali, na wataalamu ili kuongeza ukuaji endelevu wa utalii miongoni mwa nchi za G20.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Utalii ya Afrika Kusini, mkutano huo unaashiria mwanzo wa mfululizo wa shughuli zitakazofanyika mwaka huu hadi Mkutano wa Mawaziri wa Utalii wa G20 utakaofanyika Septemba.

Wizara hiyo pia imesema vipaumbele vikuu vya utalii katika shughuli hizo za G20 ni pamoja na maendeleo ya akili mnemba yanayoweka kipaumbele kwa mahitaji ya watu, uvumbuzi wa kuhamasisha safari za watalii, na kampuni mpya za utalii na zile ndogo na zenye ukubwa wa kati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha