

Lugha Nyingine
AU kuanzisha Shirika la Usalama wa Chakula Afrika ili kuimarisha viwango vya bara zima
Umoja wa Afrika (AU) umetangaza kuanzisha Shirika la Usalama wa Chakula Afrika hivi karibuni katika jitihada za kuimarisha usalama wa chakula katika bara zima.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana Jumatano, AU imesema kuwa shirika hilo litatumika kama taasisi yake maalum ya kiufundi, inayoratibu sera na kanuni za usalama wa chakula, na mifumo ya tathmini ya hatari kote barani Afrika.
Wakati wa Mkutano wa 38 wa Kawaida wa Baraza la Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU, ambao ulifanyika Februari mjini Addis Ababa, Ethiopia, AU ilipitisha sheria ya kuanzishwa kwa Shirika la Usalama wa Chakula Afrika.
Taarifa hiyo imenukuu Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema, hatua hiyo ni ya kuwa na mwitikio kwa mzigo mkubwa wa Afrika wa magonjwa yanayotokana na chakula, ambayo yanaathiri watu milioni 91 na kusababisha vifo 137,000 kwa mwaka, ikiwa ni theluthi moja ya vifo vinavyotokana na magonjwa yanayosababishwa na chakula duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma