Abiria milioni 14.8 wasafirishwa kwa reli ya SGR ya Kenya tangu izinduliwe

(CRI Online) Machi 06, 2025

Abiria zaidi ya milioni 14.8 wamesafirishwa kwa reli ya SGR ya Kenya kati ya Nairobi na Mombasa tangu reli hiyo izinduliwe mwezi Juni mwaka 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumanne na Kampuni ya Uendeshaji wa Reli ya Africa Star (AfriStar), ambayo ni mwendeshaji wa reli hiyo ya SGR, hadi kufikia tarehe 28 Februari, licha ya abiria hao waliosafirishwa, reli ya mizigo ya SGR pia imesafirisha makontena milioni 3.018 ya futi 20 (TEUs) na bidhaa za tani milioni 38.47.

Pia siku 2,831 za uendeshaji salama wa reli hiyo ya SGR zimerekodiwa na AfriStar, kampuni ambayo inaweka lengo la zaidi ya hapo.

Shirika la Reli Kenya (KRC) limesema katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka 2024, mapato ya reli hiyo ya abiria ya SGR yameongezeka kwa asilimia 36 licha ya kupungua kwa uchukuzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha