Treni ya mwendo kasi zaidi duniani yafanyiwa majaribio ya mahitaji ya muundo wake mjini Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2025

Picha hii ikionyesha treni ya mwendokasi ya CR450AF mjini Beijing, mji mkuu wa Uchina, Desemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

Picha hii ikionyesha treni ya mwendokasi ya CR450AF mjini Beijing, mji mkuu wa Uchina, Desemba 29, 2024. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING – Treni za mwendokasi zaidi duniani za miundo kielelezo ya awali, za CR450, zenye kasi ya majaribio ya hadi kilomita 450 kwa saa na kasi ya uendeshaji ya kilomita 400 kwa saa, sasa zinafanyiwa majaribio ya kukidhi mahitaji ya miundo kwenye reli ya mzunguko ya Beijing kwa ajili ya huduma za kibiashara siku zijazo.

Treni hizo mpya zilioneshwa kwa mara ya kwanza kwa umma mjini Beijing Desemba 29, 2024. Zina kasi zaidi kuliko treni za mwendo kasi za Fuxing za CR400 zinazofanya kazi kwa sasa, ambazo zinafanya kazi kwa kasi ya kilomita 350 kwa saa.

Wang Feng, makamu mkuu wa kampuni mzalishaji wa treni hizo,Shirika la CRRC, amesisitiza kuwa CR450 inawakilisha kiwango kikubwa cha mafanikio katika nadharia, teknolojia, vifaa, viwango, na usimamizi wa uendeshaji ya treni ya mwendo kasi, Jarida la Sayansi na Teknolojia limeripoti jana Alhamisi.

“Ili kufikia kasi isiyo na kifani ya uendeshaji wa kilomita 400 kwa saa, wahandisi waliboresha uwezo wa mvutano, ufanisi kamili, na mifumo ya pantografu,” Wang ameeleza.

Wang ameeleza kuwa, treni hiyo inatumia mfumo wa mvutano wa kudumu wa sumaku uliopozwa na maji, bogie ya kizazi kipya yenye utulivu wa hali ya juu, na ubunifu wa mifumo mingi ili kuendeleza uendeshaji wake wa kasi ya juu.

Mfanyakazi akifanya majaribio katika treni ya mwendokasi ya CR450 ya muundo kielelezo wa awali mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 25, 2025. (Xinhua/Li Xin)

Mfanyakazi akifanya majaribio katika treni ya mwendokasi ya CR450 ya muundo kielelezo wa awali mjini Beijing, mji mkuu wa China, Februari 25, 2025. (Xinhua/Li Xin)

“Usalama unaimarishwa na teknolojia ya ngazi mbalimbali ya udhibiti wa breki na vihisi fuatiliaji zaidi ya 4,000 ndani ya treni. Hii hufuatilia mifumo muhimu, ikijumuisha gia za kukimbia, bodi la treni, pantografu zenye voltage ya juu, udhibiti wa treni na mifumo ya kutambua moto, kwa wakati halisi. Mfumo wa juu wa upeo pia umeongeza utambuzi wa dharura wa njia za reli” amesema.

Amebainisha, kuhusu uokoaji nishati, muundo ulioboreshwa wa kujongea kwenye bogi hupunguza kwa kiasi kikubwa ukinzani wa hewa, wakati huohuo teknolojia na nyenzo mpya nyepesi hupunguza uzito wa treni kwa asilimia 10 na kupunguza ukinzani wa kukimbia kwa asilimia 22.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha