

Lugha Nyingine
China kutoa uhakika kwa Dunia isiyo na uhakika: Waziri wa Mambo ya Nje wa China
(Mpiga picha:Liu Dawei/Xinhua)
BEIJING - China itatoa uhakika kwa dunia hii isiyo na uhakika, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi Wang ameuambia mkutano na waandishi wa habari mapema leo Ijumaa pembezoni mwa mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la China unaoendelea mjini Beijing.
"Tunaishi kwenye dunia inayobadilika na yenye misukosuko, ambapo uhakika unazidi kuwa rasilimali adimu," amesema
"Diplomasia ya China itasimama bila kuyumba kwenye upande sahihi wa historia na upande wa upigaji hatua wa binadamu. Tutatoa uhakika kwa dunia hii isiyo na uhakika," amesema.
Wang amesema China itakuwa nguvu yenye usawa na ya haki kwa ajili ya amani na utulivu duniani, nguvu ya kimaendeleo kwa haki na usawa wa kimataifa, na nguvu ya kiujenzi kwa ajili ya maendeleo ya pamoja ya dunia.
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa China amesema, nchi hiyo itashikilia ushirikiano wa kweli wa pande nyingi na kulinda mfumo wa biashara huria wa pande nyingi.
"Tutaendelea kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, na kuchangia fursa kubwa za ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na nchi zote," Wang amesema.
Watu mjini Lhasa, China wafanya maandalizi ya sikukuu ijayo ya Mwaka Mpya wa Watibet
Mandhari na wanyama katika Hifadhi ya Taifa ya Nairobi, Kenya
Habari Picha: Kituo cha Matengenezo yote ya Ndege katika sehemu moja mjini Haikou, China
Dunhuang katika Mkoa wa Gansu wa China yakaribisha maendeleo mapya
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma