Viongozi wa Cote d'Ivoire na Ghana wajadili uhusiano na ushirikiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2025

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (Kulia) akimkaribisha Rais wa Ghana John Dramani Mahama mjini Abidjan, Cote d'Ivoire, Machi 5, 2025. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (Kulia) akimkaribisha Rais wa Ghana John Dramani Mahama mjini Abidjan, Cote d'Ivoire, Machi 5, 2025. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

ABIDJAN - Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara na mwenzake wa Ghana, John Dramani Mahama, wamejadili uhusiano na ushirikiano wa pande mbili mjini Abidjan siku ya Jumatano, na wamesisitiza haja ya Mali, Burkina Faso na Niger kubaki katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Kwa mujibu wa ikulu ya Cote d'Ivoire, Ouattara na Mahama wamekita mjadala wao katika maslahi ya pamoja, ikiwemo ulinzi, usalama, uchumi wa kakao (nchi zote mbili ni wazalishaji wakuu duniani), madini, nishati, na miradi mikubwa ya ECOWAS, kama vile Ukanda wa Abidjan-Lagos na pendekezo la sarafu ya pamoja, ECO.

Pia wameahidi kuunga mkono utekelezaji wa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kimkakati wa Cote d'Ivoire-Ghana wa 2017.

Mahama, ambaye aliwasili Abidjan mapema siku hiyo, amesisitiza kwamba raia wa Cote d'Ivoire na Ghana ni "watu wamoja" na akahimiza mataifa yote mawili kuendelea kushirikiana. Pia amehimiza uhusiano thabiti wa kiuchumi ili kuimarisha mchango wao ndani ya Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, lenye makao yake makuu mjini Accra, Ghana.

Wamesisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano katika usalama na ulinzi ili kuhakikisha amani na utulivu katika Afrika Magharibi, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ugaidi, uharamia wa baharini na aina nyingine za biashara haramu katika eneo hilo.

Kwenye mkutano uliofuata na waandishi wa habari, wamezungumzia hali ya kijamii na kisiasa nchini Mali, Burkina Faso na Niger – nchi tatu wanachama wa Muungano wa Nchi za Sahel (AES), ambazo zilijiondoa kutoka ECOWAS Januari 2024. Marais wote wawili wamesisitiza umuhimu wa kutoa usaidizi kwa mataifa hayo ili kushughulikia mahitaji ya kibinadamu na usalama.

Ouattara ameonyesha kuamini uwezo wa mwenzake wa Ghana wa kuzishawishi nchi hizo tatu kubakia katika ECOWAS, akisema kuwa "ni muhimu kwa mustakabali wa watu wa Afrika Magharibi."

"Natoa wito kwa nchi za AES: tuko imara zaidi tukiwa mataifa 15 kuliko mataifa matatu," ameongeza.

Kwa upande wake, Mahama ameahidi kushughulikia suala hilo “katika njia bora zaidi,” akisisitiza hali ya kutegemeana kiuchumi ya eneo hilo, na changamoto zinazokabili raia wa nchi hizo wanaoishi Cote d'Ivoire na mataifa mengine ya ECOWAS kutokana na vizuizi vya mipaka. 

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (Kulia) akifanya mazungumzo na Rais wa Ghana John Dramani Mahama mjini Abidjan, Cote d'Ivoire, Machi 5, 2025. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (Kulia) akifanya mazungumzo na Rais wa Ghana John Dramani Mahama mjini Abidjan, Cote d'Ivoire, Machi 5, 2025. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (Kulia) akishikama mkono na Rais wa Ghana John Dramani Mahama kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Abidjan, Cote d'Ivoire, Machi 5, 2025. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara (Kulia) na Rais wa Ghana John Dramani Mahama wakihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Abidjan, Cote d'Ivoire, Machi 5, 2025. (Picha na Yvan Sonh/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha