

Lugha Nyingine
Sudan yakaribisha hatua ya UNSC kukataa mamlaka ya pamoja
Serikali ya Sudan siku ya Alhamisi ilikaribisha taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) ya kukataa kutiwa saini mkataba unaolenga kuunda mamlaka ya pamoja nchini humo.
Kupitia taarifa ya waziri wa habari wa Sudan ambaye pia ni msemaji wa serikali, Khalid Ali Aleisir, amesisitiza azma ya serikali ya kutafuta suluhu ambazo zitahakikisha mgogoro huo unamalizika, kulinda umoja na ukamilifu wa ardhi ya Sudan, na kutimiza matarajio ya watu wake ya kuwepo kwa usalama, demokrasia na maendeleo.
Aidha amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kusaidia walioathirika na vita akisisitiza dhamira ya serikali katika kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu.
Siku ya Jumatano katika taarifa UNSC ilieleza "wasiwasi mkubwa" juu ya kutiwa saini kwa mkataba wa kuanzisha mamlaka ya pamoja nchini Sudan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma