Kampuni ya Huawei yahimiza mageuzi ya kidigitali ya Uganda kupitia mipango ya TEHAMA

(CRI Online) Machi 07, 2025

Kampuni ya Huawei ya China inahimiza mageuzi ya kidigitali ya Uganda kupitia mipango mbalimbali, wakati nchi hiyo ikiharakisha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

Ripoti ya Uwajibikaji wa Kijamii Kwa Kampuni ya Kibiashara ya Mwaka 2024 iliyotolewa Jumatano na kampuni hiyo inasisitiza juhudi zake katika kuhimiza elimu ya kidigitali, kuunga mkono jamii za wenyeji, na kujenga mfumo endelevu wa ikolojia ya TEHAMA.

Moja ya mpango muhimu wa Huawei, Mradi wa DigiTruck unalenga kutoa mafunzo kwa watu zaidi ya elfu kumi wa Uganda ndani ya miaka mitatu.

Mradi huo ulioanzishwa mwaka 2023, hadi sasa umenufaisha watu zaidi ya elfu sita hasa kwenye maeneo ya mbali kupitia mafunzo ya kidigitali kwa kutumia lori linalobeba darasa la kidigitali lililoundwa kwa makontena.

Maofisa wa serikali ya Uganda wamepongeza mradi huo wakisisitiza kuwa unaendana na Dira ya Mwaka 2040 ya Uganda na Mpango wa Maendeleo wa Nchi, ambavyo vyote vinaweka kipaumbele katika uchumi wa kidigitali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha