EAC yazindua kaulimbiu ya "Tembelea Afrika Mashariki" kwenye Maonesho ya utalii mjini Berlin ili kukuza utalii

(CRI Online) Machi 07, 2025

Mamia ya wadau wa utalii wanaohudhuria Maonesho ya Utalii ya Kimataifa (ITB) mjini Berlin, Ujerumani wameshuhudia uzinduzi wa kaulimbiu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) "Tembelea Afrika Mashariki: Upate Furaha".

Kwenye taarifa iliyotolewa katika makao makuu yake mjini Arusha, Tanzania, EAC imesema kuwa mpango huo muhimu unalenga kutangaza kwa pamoja EAC kama kivutio kimoja cha utalii.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa wadau wa utalii wamekaribisha hatua hiyo, wakisema ni hatua kubwa ya kuimarisha utalii wa kikanda na kuhakikisha shughuli endelevu za utalii.

Chini ya kaulimbiu hiyo ya "Tembelea Afrika Mashariki: Upate Furaha", jumuiya hiyo si tu inaonyesha uzuri na utajiri wake wa kiutamaduni, bali pia inaimarisha mwonekano wa Afrika Mashariki kama maeneo yenye vivutio mbalimbali vya kipekee.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha