China kuweka ushuru wa ziada kwa baadhi ya bidhaa za Canada baada ya uchunguzi dhidi ya kubagua bidhaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2025

BEIJING - China imetangaza leo Jumamosi kwamba itaweka ushuru wa ziada kwa baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Canada kwenye msingi wa uamuzi wa uchunguzi dhidi ya kubagua bidhaa.

Serikali ya China imesema, mara moja kuanzia Machi 20, ushuru wa ziada wa asilimia 100 utatozwa kwa mafuta ya rapa, keki za mafuta na mbaazi zinazotoka Canada, huku bidhaa za baharini na nyama ya nguruwe zikitozwa ushuru wa ziada wa asilimia 25.

Uamuzi huo umekuja baada ya uchunguzi wa China dhidi ya kubagua bidhaa, ambao umebaini kuwa hatua zuizi za Canada dhidi ya baadhi ya bidhaa za China zimevuruga utaratibu wa kawaida wa biashara na kuathiri haki na maslahi halali ya kampuni za China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha