Wajumbe wa Bunge la umma la China walaani vikwazo vya Marekani kwa Xinjiang, wakaribisha ziara

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 08, 2025

BEIJING - Wajumbe wa bunge la umma la China kutoka Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang wa China wamelaani vikwazo vya Marekani dhidi ya Mkoa huo kwa kisingizio cha kile kinachoitwa "kutumikishwa kazi kwa lazima." Pia wamekaribisha watu kutoka kote duniani kuona Xinjiang halisi kwa macho yao wenyewe.

Wanahabari takriban 100 wa China na ng'ambo kutoka vyombo vya habari zaidi ya 70 jana Ijumaa walihudhuria mjadala wa wazi wa wajumbe hao wa Xinjiang kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China.

Akizungumzia kile kinachoitwa "Sheria ya Sera ya Haki za Kibinadamu ya Wauygur" na "Sheria ya Kuzuia Kutumikishwa Kazi kwa Lazima ya Wauygur" za Marekani, Ma Xingrui, mjumbe wa Bunge hilo la 14 ambaye pia ni katibu wa kamati ya Mkoa huo wa Xinjiang ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema nyaraka hizo mbili "zinalenga kuzuia maendeleo ya Xinjiang na kutumbukiza Mkoa huo katika umaskini na hali ya kuwa nyuma, ambayo inaweza kuzalisha kujitenga ambako kunazuia maendeleo ya China."

Akibainisha kuwa Mkutano wa Vyombo vya Habari Duniani mwaka jana katika Urumqi, mji mkuu wa Mkoa huo, ulikaribisha wawakilishi 200 kutoka vyombo vya habari vya nchi mbalimbali zaidi ya 100, Ma amesema waandishi hao wa habari wa kigeni walifanya uchunguzi wa kimatembezi na hojaji katika mkoa mzima, na uchunguzi wao haukuonyesha ushahidi wowote unaothibitisha madai ya "kutumikishwa kazi kwa lazima" au "mauaji ya kimbari."

"Ninaalika waandishi wa habari wa kimataifa kuanza uchunguzi wa matembezi na hojaji katika mkoa mzima ili kuona Xinjiang halisi, badala ya kufumbwa macho na baadhi ya vyombo vya habari vinavyolenga kukashifu Xinjiang," ameongeza.

Wang Mingshan, mjumbe mwingine wa Bunge hilo ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la Xinjiang, amesema vikwazo hivyo vilivyowekwa na baadhi ya nchi kwa kisingizio cha "Kutumikishwa kazi kwa lazima" vimekiuka kwa kiasi kikubwa haki na maslahi ya kampuni za Xinjiang, hivyo kusababisha "kulazimishwa ukosefu wa ajira" na "kulazimishwa umaskini."

Amesema, kwa mujibu wa Shirika la Kazi la Kimataifa, ufafanuzi wa "Kutumikishwa kazi kwa lazima" unahusisha mambo matatu: "tishio la adhabu yoyote," "kutotaka mwenyewe" vilevile "kazi au huduma."

"Watu wa makabila yote wanaweza kuchagua wapi pa kufanya kazi na nini cha kufanya kutokana na utashi wao," amesema Wang. "Kile kinachoitwa 'Kutumikishwa kazi kwa lazima' mkoani Xinjiang ni pendekezo la uwongo dhahiri." Ameongeza.

Baada ya kuzuru Xinjiang mwaka jana, Alena Douhan, Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu athari mbaya za hatua shurutishi za upande mmoja katika kufurahia haki za binadamu, alisema vikwazo hivyo vya upande mmoja vinatishia haki za makundi ya watu wanaowezekana zaidi kudhuriwa nchini China na kutaka vikwazo hivyo viondolewe.

"Xinjiang kamwe haitaruhusu inyonywe, au kukandamizwa," amesema Wang, akiongeza kuwa azimio la mwaka 2024, lililopitishwa na mkoa huo linalopinga vikwazo hivyo vya Marekani, limeziwezesha kampuni kwa hatua kali za kupambana na siasa ya umwamba.

"Tunahimiza kampuni zaidi kuchukua silaha za kisheria na kutetea maslahi na haki zao halali," Wang amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha