Wajumbe na washauri wa kisiasa wa China wapinga shughuli za "kujitenga kwa Taiwan", uingiliaji wa nje

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 09, 2025

BEIJING - Wajumbe na washauri wa kisiasa wa Kitaifa wenye asili ya Taiwan wametoa utambuzi wao wa sehemu zinazohusu Taiwan katika ripoti ya kazi ya serikali ya China na kupaza sauti ya upingaji wao thabiti kwa shughuli za "Kujitenga kwa Taiwan" na uingiliaji wa nje.

Ripoti hiyo inajadiliwa katika mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China, au bunge kuu la China.

"Tutapinga kithabiti shughuli za kujitenga zinazolenga 'Taiwan Kujitenga’ na uingiliaji wa nje, ili kuhimiza maendeleo ya amani ya uhusiano wa pande mbili za Mlango Bahari," inasema ripoti hiyo ya kazi.

Zhou Qi, mjumbe wa Bunge hilo na makamu mkuu wa Shirikisho Kuu la China la Watu wa Taiwan, amesema wajumbe walipiga makofi wakati sehemu hizo zinazohusu Taiwan zikisomwa wakati ripoti hiyo ya kazi ikiwasilishwa kwa ajili ya kupitiwa na wajumbe siku ya Jumatano kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing.

Ilikuwa ni kielelezo cha "shauku yetu kubwa kwa muungano wa kitaifa," Zhou amesema.

"Muungano wa kitaifa ni matarajio ya pamoja ya watu wote wa China," amesema Zou Zhenqiu, mjumbe wa bunge hilo, ambaye pia ni makamu mkuu wa Shirikisho Kuu la China la Watu wa Taiwan.

Ripoti hiyo ya kazi ya serikali imeonyesha uaminifu wa China Bara katika kufanya kila juhudi kuelekea muungano wa amani, amesema Li Xingkui, mjumbe wa Bunge hilo mwenye mizizi ya familia mjini Taichung, katikati mwa Taiwan.

Ripoti hiyo ya kazi ya serikali pia inajadiliwa na wajumbe wa Kamati ya 14 ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC), au chombo cha juu cha mashauriano ya kisiasa cha China, katika mkutano wake wa mwaka.

Wang Yu, mjumbe wa Kamati ya hiyo ya Kitaifa ya CPPCC, amesema kuwa shughuli za kujitenga Taiwan na uingiliaji wa nje unaolenga kuzuia maendeleo ya amani ya uhusiano wa pande mbili za Mlango-Bahari haviwezi kurudisha nyuma mchakato wa muungano.

Chen Wei, mjumbe mwingine wa Kamati hiyo ya Kitaifa ya CPPCC, ameonya juu ya hatari ya shughuli za kujitenga kwa Taiwan na kutoa wito kwa watu wa Taiwan kuchukua hatua ili kulinda amani na utulivu katika pande za Mlango Bahari.

Wang na Chen wote ni wanachama wa Taiwan Democratic Self-Government League, mojawapo ya vyama vinane visivyo vya kikomunisti nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha