Kikao cha tatu cha Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China chafungwa Beijing

(CRI Online) Machi 10, 2025

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)

Kikao cha tatu cha Baraza la 14 la Mashauriano ya Kisiasa la China (CPPCC) kimefungwa leo hapa Beijing baada ya kukamilisha ajenda mbalimbali.

Mkutano wa ufungaji wa kikao kicho umepitisha azimio kuhusu ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya baraza hilo, azimio kuhusu ripoti ya kazi ya ushughulikiaji wa mapendekezo tangu kikao cha pili cha baraza hilo, ripoti ya uchunguzi wa mapendekezo ya kikao kicho iliyowasilishwa na kamati inayoshughulikia mapendekezo ya baraza hilo, na azimio la kisiasa la kikao hicho.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha