

Lugha Nyingine
Wajumbe wa Bunge la Umma la China wawasilisha mapendekezo 269 kwenye mkutano wa mwaka wa bunge hilo
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye ofisi ya sekretarieti ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 9, 2025. (Xinhua/Zheng Huansong)
BEIJING – Watunga sheria wa kitaifa wa China wamewasilisha mapendekezo 269 hadi Machi 8 ambayo ni tarehe ya mwisho kuwasilisha mapendekezo kwa mkutano mkuu wa tatu unaoendelea mjini Beijing wa Bunge la Umma la 14 la China, ambao ni mkutano wa mwaka wa chombo hicho kikuu cha utungaji wa sheria.
Ofisi ya Sekretarieti ya mkutano huo imesema jana Jumapili kwamba ilikuwa imepokea maoni na mapendekezo zaidi ya 8,000 kutoka kwa wajumbe wa Bunge hilo.
Ofisi ya sekretarieti hiyo imesema “kati ya maoni na mapendekezo hayo, 268 yanahusu kazi ya kutunga sheria na moja linahusu kazi ya usimamizi”, na mapendekezo hayo yanahusu utungaji sheria katika maeneo muhimu, yanayoibukia na mambo yanayohusika na nchi za nje.
Ofisi hiyo imesema, mapendekezo hayo yanahusu mada mbalimbali, zikiwemo kuongeza matumizi kwenye manunuzi, kuhimiza matumizi ya AI ili kuendeleza ukuaji uchumi, na kulinda haki na maslahi ya viwanda na kampuni binafsi.
Ofisi ya Sekretarieti hiyo imeeleza kuwa, inapitia kwa kina mapendekezo hayo na itatayarisha ripoti juu ya kuyashughulikia ili kuiwasilisha kwa Tume ya Utendaji wa mkutano huo wa tatu ili kujadiliwa kwenye mkutano.
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye ofisi ya sekretarieti ya mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China mjini Beijing, Machi 9, 2025. (Xinhua/Zheng Huansong)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma