

Lugha Nyingine
Iran yakataa mazungumzo kuvunja mpango wake wa “nyuklia kwa matumizi ya amani”
Ujumbe wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa umesema, majadiliano yenye lengo la kuvunja mpango wake wa matumizi ya nyuklia kwa amani "kamwe hayatafanyika".
Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X, zamani Twitter jana Jumapili, ujumbe huo wa Iran umesema kuwa Iran inaweza kufikiria kufanya mazungumzo yanayolenga kuondoa wasiwasi juu ya uwezekano wa mpango huo wa nyuklia wa Iran kuwa wa kijeshi lakini umekataa mazungumzo yoyote yenye lengo la kuondoa mpango wake wa nyuklia kwa shughuli za kiraia.
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei awali siku ya Jumamosi alisema, madhumuni ya baadhi ya nchi kushikilia kufanya mazungumzo si kwa ajili ya kutatua matatizo, bali ni kuweka nia zao kwa nchi nyingine, na Iran kamwe haitakubali.
Hayo yamekuja wakati ambapo, Rais wa Marekani Donald Trump kwenye mahojiano na kituo cha Habari cha Fox news yaliyorushwa Ijumaa, mwishoni mwa wiki alisema amemtumia barua Bw. Khamenei akiihimiza Iran kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu kuacha mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia, lakini Ujumbe huo wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa umesema bado haujapokea barua hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma