Kundi la madaktari wa China lakamilisha mradi wa kwanza wa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi nchini Sierra Leon

(CRI Online) Machi 10, 2025

Hafla ya uzinduzi wa ripoti ya matokeo ya mradi wa kwanza wa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi nchini Sierra Leone imefanyika hivi karibuni kwenye makao ya Wizara ya Afya ya nchi hiyo.

Hafla hiyo maalum ilikuwa na lengo la kulitunukia Kundi la 25 la timu ya madaktari wa China (Hunan) kwa mchango wake mkubwa wa kuiunga mkono Sierra Leone katika juhudi za kuzuia saratani ya mlango wa kizazi nchini humo.

Ofisa mwandamizi wa matibabu wa Wizara ya Afya ya Sierra Leone Bw. Sartie M.Kenneh amewashukuru madaktari hao kwa mchango wao katika kuhakikisha afya za wananchi wa nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha