

Lugha Nyingine
Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China watoa msukumo muhimu kwa maendeleo ya Afrika
Mkurugenzi wa Shirika la Habari la nchini Senegal Momar Diongue amesema, Mikutano Mikuu Miwili ya China inayoendelea mjini Beijing imeonyesha dunia jinsi nchi kubwa yenye watu bilioni 1.4 inavyoweza kupata maendeleo endelevu kupitia mipango ya kisayansi.
Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni, Bw. Diongue amesema, viongozi wa China wamekuwa na maono ya mbali na kuwaongoza Wachina kufanya kazi kwa bidii na kuondokana na matatizo mengi ili kufikia mafanikio ya maendeleo ya leo.
Amesema Afrika inatarajia kushirikiana na China kushughulikia kwa pamoja changamoto za kimataifa na kuhimiza kufikiwa kwa malengo ya maendeleo endelevu, huku akiongeza kuwa China imetoa uungaji mkono muhimu kwa Afrika na ushirikiano kati ya pande hizo mbili umepata mafanikio makubwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma