

Lugha Nyingine
Wasimamizi wa amani watoa wito wa uchunguzi wa haraka wa vurugu zilizotokea Sudan Kusini
Wasimamizi wa amani nchini Sudan Kusini wametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka kufuatia vurugu zilizotokea Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Jimbo la Upper Nile na shambulio dhidi ya helikopta ya Umoja wa Mataifa lililosababisha kifo cha ofisa mmoja wa Umoja huo na askari kadhaa.
Tume ya Pamoja ya Usimamizi na Tathmini imelaani vikali vurugu hizo zilizotokea Upper Nile na shambulio hilo dhidi ya helikopta ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) wakati wa jukumu la uokoaji katika Kaunti ya Nasir, na kuzitaka pande zinazopigana kuacha mapigano na kufanya mazungumzo ili kuleta amani nchini humo.
Mapigano hayo katika mji wa Nasir yameongeza mvutano tangu Jumatatu wiki iliyopita, na kusababisha kukamatwa kwa maofisa wa ngazi ya juu wa serikali na jeshi kutoka kundi la upinzani la SPLM/A-IO linaloongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Riek Machar.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma