

Lugha Nyingine
China yazindua kituo cha uvumbuzi kwa majaribio ya vifaa vya teknolojia ya hali ya juu
Picha hii iliyopigwa Februari 20, 2025 ikionyesha roboti fuatiliaji katika Kampuni ya Teknolojia ya kisasa ya Tianjin SIASUN kwenye Mji wa Kiteknolojia wa Zhongguancun wa Beijing-Tianjin mjini Tianjin, kaskazini mwa China. (Xinhua/Sun Fanyue)
BEIJING - China hivi karibuni imezindua kituo cha kitaifa cha uvumbuzi kwa majaribio yasiyoharibifu ya vifaa vya teknolojia ya hali ya juu (NDT) mjini Beijing, ikilenga kuendeleza teknolojia za AI za ukaguzi ili kuunga mkono sekta mahiri ya viwanda ya nchi hiyo.
Kituo hicho kikiwa chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Soko ya China na kimsingi kikiungwa mkono na kituo cha utafiti na majaribio ya teknolojia ya ulinzi na majaribio cha Shirika la Sayansi na Tasnia ya Vyombo vya Anga la China (CASIC), kinajikita katika utafiti wa teknolojia za kisasa, za kimapinduzi na za kawaida katika majaribio yasiyoharibifu ya vifaa vya teknolojia ya hali ya juu, shirika la habari la China, Xinhua limeripoti likirejelea habari iliyoripotiwa na gazeti la People's Daily jana Jumatatu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kituo hicho kinatafuta kuunda jukwaa shirikishi ambalo linajumuisha pamoja tasnia, taaluma na utafiti.
"Pamoja na maendeleo ya haraka ya vifaa vya kisasa vya teknolojia ya hali ya juu, kama vile bidhaa za vyombo vya anga, vifaa vya nguvu za nyuklia, na miundo mikubwa ya madaraja, matumizi ya nyenzo mpya, michakato, na viwanda vya teknolojia za AI vimeleta mfululizo wa changamoto za ufuatiliaji na tathmini," Li Hongmin, mwenyekiti wa kituo hicho cha uvumbuzi na mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa teknolojia ya ulinzi na majaribio cha CASIC.
"Kituo cha uvumbuzi kitashughulikia mapengo katika nyanja hizi kwa kutengeneza teknolojia za hali ya juu za NDT huku kikiimarisha matumizi yake ya AI katika taarifa na viwango," Li ameongeza.
Kituo hicho cha uvumbuzi kinaleta pamoja taasisi ongozi 46, zikiwemo Chuo Kikuu cha Xi'an Jiaotong, Taasisi ya Teknolojia ya Harbin, na Taasisi ya Ukaguzi na Utafiti wa Vifaa Maalumu ya China, zikiunda muungano shirikishi ili kuhimiza mafanikio mapya ya kiteknolojia na kuinua viwango vya tasnia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma