

Lugha Nyingine
Tume ya utendaji wa mkutano wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China yafanya kikao cha tatu
Akiwa amekabidhiwa kazi na Zhao Leji, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, Li Hongzhong, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano akiongoza kikao cha tatu cha tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei)
BEIJING – Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China, ambalo ni chombo cha utungaji wa sheria cha kitaifa cha China, imefanya kikao chake cha tatu jana Jumatatu, ambapo akiwa amekaimishwa kazi na Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano Li Hongzhong ameongoza kikao hicho.
Kikao hicho kimeamua kuwasilisha mswada wa azimio kuhusu marekebisho ya Sheria ya Wajumbe wa Bunge la Umma la China na wale wa Mabunge ya Serikali za Mitaa katika Ngazi Mbalimbali kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la Umma la 14 la China unaondelea ili kupigiwa kura.
Kikao hicho kimeamua kuwasilisha nyaraka tatu kwenye mkutano huo wa mwaka wa Bunge la Umma ili kujadiliwa na kupitishwa kwa nyaraka hizo. Nyaraka hizo ni miswada ya maazimio kuhusu ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma, Mahakama Kuu ya Umma ya China na Idara Kuu ya Uendeshaji Mashtaka ya China.
Kikao hicho pia kimesikiliza na kupitisha ripoti ya kushughulikiwa kwa mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe wa Bunge hilo kwenye mkutano wake huo wa mwaka.
Wenyeviti watendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano walikutana kabla ya kikao hicho kuandaa nyaraka.
Akiwa amekabidhiwa kazi na Zhao Leji, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano wa tatu wa Bunge la 14 la Umma la China ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Umma la China, Li Hongzhong, mwenyekiti mtendaji wa Tume ya Utendaji ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la 14 la Umma la China, akiongoza kikao cha pili cha wenyeviti watendaji wa Tume ya Utendaji wa mkutano kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 10, 2025. (Xinhua/Pang Xinglei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma