

Lugha Nyingine
Kenya yatoa hifadhi kwa wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi zaidi ya 800,000
Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Kenya Kipchumba Murkomen amesema, kwa sasa Kenya inatoa hifadhi kwa wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi 829,211, ikiwa ni ongezeko kutoka watu 823,932 mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na wanahabari mjini Nairobi, Waziri Murkomen amesema wengi wa wakimbizi wanatoka nchi zilizo ndani ya Maziwa Makuu, Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, ambazo zinashuhudia mapigano yanayolazimisha watu wengi kukimbia makazi yao.
Amesema ongezeko la wakimbizi limesababisha kuongezeka kwa mahitaji, ikiwemo usalama, chakula, makazi, elimu, na huduma za afya pamoja na usaidizi katika kujikimu kimaisha.
Pia amesema, ongezeko la wakimbizi halipaswi kuwa mzigo wa Kenya pekee bali wajibu wa jumla wa jamii ya kimataifa, na kuongeza kuwa, ili kuboresha upatikanaji wa huduma za serikali, Kenya imeanzisha kituo cha takwimu kitakachotoa takwimu sahihi za wakimbizi kwa ajili ya kupanga na kusimamia usalama wa taifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma