Viongozi wa Niger na Ghana waahidi kushirikiana kupambana na ugaidi

(CRI Online) Machi 11, 2025

Mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi wa Taifa nchini Niger Bw. Abdourahamane Tchiani Jumapili alikutana na Rais wa Ghana John Mahama, ambaye yuko ziarani nchini Niger, na viongozi hao wawili wamesema nchi hizo mbili zitashirikiana kupambana na ugaidi.

Viongozi hao wamebadilishana maoni kuhusu matishio ya ugaidi yanayoikabili kanda ya Sahel, magharibi mwa Afrika, na kusema matishio hayo yamezuia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya serikali za nchi mbalimbali, na nchi hizo mbili zitashirikiana kupambana na ugadi kwa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha