

Lugha Nyingine
IGAD kufanya mkutano kwa njia ya mtandao kujadili mgogoro wa Sudan Kusini
Mamlaka ya Kiserikali kuhusu Maendeleo ya Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) inatarajia kufanya mkutano wake wa 43 wa Kilele wa Wakuu wa Nchi na Serikali leo Jumatano kwa njia ya mtandao ili kujadili hali inayobadilika ya nchini Sudan Kusini kufuatia mgogoro wa kiusalama nchini humo.
Katika taarifa yake, IGAD imesema imeshikilia dhamira yake ya kutumia mazungumzo, kupunguza mvutano, na kutafuta suluhu ya amani kwa watu wa Sudan Kusini.
Mapigano makali yameibuka katikati ya mwezi Februari kati ya Jeshi la Sudan Kusini na makundi ya kiraia yenye silaha katika Kaunti ya Nasir nchini humo, na mvutano huo umeongezeka zaidi baada ya serikali kutangaza mpango wa kupeleka vikosi vipya katika kaunti hiyo kuchukua nafasi ya vikosi vilivyokuwepo kwa miaka mingi katika kaunti hiyo.
Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa IGAD Workneh Gebeyehu alitoa wito wa kujizuia na mazungumzo ili kupunguza mvutano unaoongezeka nchini Sudan Kusini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma