Utafiti wabaini ukame mkali katika Pembe ya Afrika mwaka 2021- 2022 ulihusiana na shughuli za kibinadamu

(CRI Online) Machi 12, 2025

Wanasayansi wamesema kuwa mabadiliko ya tabianchi yaliyotokana na shughuli za kibinadamu yaliongeza ukali wa ukame katika Pembe ya Afrika mwaka 2021 mpaka 2022.

Katika utafiti uliofanywa na wanasayansi kutoka Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya (KMD), Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine, mabadiliko ya tabianchi yamebainika kuongeza ukali wa ukame, ukosefu wa usalama wa chakula, uhaba wa maji, na shughuli za kimaisha katika kanda hiyo.

Utafiti huo umebaini kuwa, kuanzia mwezi Oktoba, 2020 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2023, kanda ya Afrika Mashariki ilishuhudia misimu mitano ya uhaba wa mvua, na kusababisha hali mbaya zaidi ya ukame katika miongo mitano.

Ukame huo pia ulisababisha mavuno hafifu, vifo vya mifugo, uhaba wa maji na vurugu, ukiwaacha watu karibu milioni 4.3 wakihitaji msaada wa kibinadamu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha