

Lugha Nyingine
Mwenyekiti wa Bunge la Umma la China apongeza waandishi wa habari kwa kuripoti mkutano wa mwaka
Zhao Leji, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Bunge la Umma la China akikutana na waandishi wa habari walioripoti habari za mkutano wa tatu wa Bunge hilo la 14, na kutoa shukrani zake kwa juhudi zao, katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2025. (Xinhua/Liu Bin)
BEIJING - Zhao Leji, Mwenyekiti wa Bunge la Umma la China jana Jumatano alikutana na waandishi wa habari walioripoti na kutangaza habari za mkutano wa tatu wa Bunge hilo la 14, akitoa shukrani zake kwa juhudi zao.
Zhao, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amepongeza vyombo vikuu vya habari kwa kutoa ripoti na kufanya utangazaji kwa maandalizi mazuri.
Amesema kuwa ripoti zao za habari zimeonesha imani na nguvu na pia zikiangazia maendeleo ya mchakato wa demokrasia uliofuata hali halisi na wenye ufanisi mkubwa.
Zhao amehimiza vyombo vya habari kuendelea kuchunguza na kutumia rasilimali tajiri za habari zinazohusika na mfumo wa Bunge la Umma la China, kazi ya Bunge la Umma la China na wajumbe wa bunge la umma, ili kusaidia kueleza vizuri simulizi ya China na demokrasia ya umma ya mchakato mzima.
Mkutano huo wa mwaka wa Bunge la 14 la Umma la China ulifanyika kuanzia Machi 5 hadi 11.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma