

Lugha Nyingine
China kuchukua hatua zote za lazima za kulinda haki na maslahi halali
BEIJING - China itachukua hatua zote za lazima za kulinda haki na maslahi yake halali, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Mao Ning amesisitiza jana Jumatano kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu swali kuhusu Rais wa Marekani Donald Trump kuweka ushuru wa ziada wa asilimia 25 kwa bidhaa za chuma na aluminiamu zinazoagizwa kutoka nje.
"China inaamini kwamba kujilinda kibiashara hakutakuwa na mbele na nyuma, na vita vya biashara na ushuru havina washindi. Hili limekuwa likitambuliwa sana katika jumuiya ya kimataifa," msemaji huyo amesema.
"Kilichofanywa na Marekani kinakiuka vibaya sheria za WTO, kuhatarisha mfumo wa biashara za pande nyingi uliowekwa kwenye msingi wa kanuni, na hakisaidii hata kidogo katika kutatua matatizo. China itachukua hatua zote za lazima ili kulinda haki na maslahi yake halali," Msemaji amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma