China yapanda msitu wenye ukubwa wa hekta karibu milioni 4.45 katika mwaka 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2025

Wakazi wakipanda miche ya miti katika  Eneo la Panlong la Mji wa Kunming, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Machi 11, 2025. (Xinhua/Chen Xinbo)

Wakazi wakipanda miche ya miti katika Eneo la Panlong la Mji wa Kunming, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, Machi 11, 2025. (Xinhua/Chen Xinbo)

BEIJING - China iliongeza juhudi zake za kupanda miti zaidi katika mwaka jana wa 2024, ambapo misitu yenye ukubwa wa hekta milioni 4.446 imepandwa nchini humu, ripoti kutoka Kamati ya Kitaifa ya Upandaji wa Miti ya China imesema jana Jumatano.

Kiwango hiki ni kikubwa zaidi kuliko upandaji wa miti wenye ukubwa wa hekta milioni 3.998 uliofikiwa mwaka 2023, kamati hiyo imesema.

China jana Jumatano iliadhimisha Siku ya Kitaifa ya Kupanda Miti kwa Mwaka wa 47.

Katika mwaka 2024 uliopita, nchi ya China pia ilirejesha hali ya awali ya mbuga zilizokuwa zimevia kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta milioni 3.224 na kuboresha hali ya ardhi ya mchanga na mawe kwenye eneo la ukubwa wa hekta milioni 2.783, ripoti hiyo imesema.

Mwaka jana, pato la jumla la shughuli za misitu, malisho na mbuga za China lilifikia yuan trilioni 10.17 (dola za kimarekani karibu trilioni 1.42) -- likiwa ni ongezeko la asilimia 9.6 kuliko mwaka 2023, ripoti hiyo imesema.

Hasa, safari za utalii wa ikolojia bilioni 2.76 zilirekodiwa katika mwaka 2024, na zimefikia ongezeko la asilimia 9.1 zaidi kuliko mwaka wa 2023, imesema ripoti hiyo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha