

Lugha Nyingine
EAC yazindua mradi wa kuboresha uzalishaji na uendelevu wa kilimo
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imezindua mradi wa Ugani wa Kilimo Endelevu cha Kikanda (ENSURE) wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 12.5 siku ya Jumanne kwa lengo la kuboresha uzalishaji na uendelevu wa kilimo katika kanda hiyo.
Katika taarifa yake iliyotolewa jana Jumatano, EAC imesema mradi huo wa miaka mitatu uliofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), unatarajiwa kuongeza uendelevu wa muda mrefu wa kilimo katika kanda hiyo kwa kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za ugani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mradi huo utajikita katika maeneo makuu matatu ambayo ni; kujenga mazingira wezeshi ya kikanda yenye uwiano kwa ugani na sera husika za kilimo, kutumia njia mbalimbali za kikanda za masuala ya ugani wa kilimo, na kuanzisha programu ya kikanda ya ujengaji uwezo katika ugani wa kilimo inayolenga kudhibiti wadudu na magonjwa ya kuvuka mpaka, hususan nzige wa jangwani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma