

Lugha Nyingine
Ukuaji wa pato la Kiuchumi la Afrika wakadiriwa kufikia asilimia 3.8 mwaka huu
(CRI Online) Machi 13, 2025
Ripoti iliyotolewa na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) imesema, ukuaji wa pato la kiuchumi la Afrika (GDP) unatarajiwa kuimarika tena, ukifikia asilimia 3.8 mwaka huu na asilimia 4.1 mwaka kesho.
Akiwasilisha ripoti hiyo, mkurugenzi wa kitengo cha uchumi mkuu, mambo ya fedha na utawala cha UNECA, Zuzana Schwidrowski amesema uchumi wa Afŕika unaendelea kuimarika, lakini ukuaji huo uko chini ya viwango ili kuendeleza maendeleo ya kijamii katika bara hilo.
Amesema hatari kwa ukuaji wa bara hilo bado ni kubwa kutokana na hali ya kutokuwa na uhakika kwenye uchumi, mgawanyiko, kupungua kwa misaada, na mivutano ya siasa za kijiografia duniani.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma