Watu 10 wauawa katika shambulizi la RSF nchini Sudan

(CRI Online) Machi 13, 2025

Takriban watu 10 wameuawa na wengine 23 kujeruhiwa katika shambulizi la makombora lililofanywa na wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) dhidi ya vitongoji vya makazi na kituo cha watu kujihifadhi katika mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini, El Fasher.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la Sudan imesema, Vikosi vya RSF pia vimefanya mashambulizi ya kutumia droni katika maeneo muhimu ndani ya mji huo wa El Fasher, lakini jeshi la anga la Sudan lilifanikiwa kutungua droni hizo.

Hakuna taarifa zozote zilizotolewa na RSF kuhusu shambulizi hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha