

Lugha Nyingine
Jitihada jumuishi za China zazaa matunda barani Afrika
Wasomi nchini Ethiopia wamesema dhamira ya China ya kuhimiza jitihada jumuishi na diplomasia ya utamaduni imezaa matunda mazuri barani Afrika.
Mtafiti katika Taasisi ya Elimu ya Sera nchini Ethiopia, Balew Demissie amesema, ushirikiano unaokua kati ya China na nchi za Afrika kupitia kuhimiza jitihada za nguvu laini za ushawishi ikiwemo mabadilishano ya kitamaduni, unaendelea kupata umaarufu kwa watu wa Afrika.
Amesema uhusiano wa kimkakati kati ya China na Afrika unaendelea kushika kasi, na kuzinufaisha pande zote mbili, kujenga dunia yenye usawa zaidi, na kubadili utaratibu wa utawala wa dunia.
Mtafiti mwandamizi wa uhusiano wa kimataifa na diplomasia katika Taasisi ya Masuala ya Kigeni ya Ethiopia, Melaku Mulualem amesema, China inatumia zaidi ya diplomasia ya utamaduni kuimarisha uhusiano wake wa kimkakati, kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia na Afrika, na jitihaza zake hizo zimepokelewa vyema na nchi nyingi za Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma